18 Jan 2015

Gabon yawika huku wenyeji wakipata sare

Wachezaji wa Gabon wakisherehekea Goli
 
Timu ya Gabon ilianza vyema kampeni yake ya kulinyakua kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuishinda Burkina Fasso na kupanda katika kilele cha kundi A.
Mchezaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubemeyang aliiweka Gabon kifua mbele kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.
Burkina Fasso walikuwa hatari kwa kipindi kirefu cha mechi hiyo kupitia wachezaji Vitesse Arnhem na mchezaji wa Chelsea anayecheza kwa mkopo Betrand Traore wakishindwa kumfunga mlinda lango Didier Ovono katika vipindi vyote viwili.
Katika mechi kati ya waandalizi wa dimba hilo Equitoial Guinea na Congo ,Thievy Bifouma alifunga bao la muda wa lala salama na hivyobasi kuinyima ushindi timu hiyo ya nyumbani katika mechi iliochezwa mbele ya mashabiki wengi katika uwanja wa Bata.

Pierr Emerick Aubamayeng

Mchezaji wa Middlesbrough Emilio Nsue aliiweka Equitorial Guinea kifua mbele katika dakika ya 16 licha ya kuonekana kwamba alikuwa ameotea.
Francis N'ganga alipiga mlingoti wa goli huku Congo wakidhibiti mpira na kufanya mashambulizi chungu nzima katika kipindi cha pili kabla ya mshambuliaji wa West Brom Thievy Bifouma kufunga katika eneo la hatari.
Congo ingeshinda mechi hiyo lakini Dominique Malonga alikosa bao la wazi.

Chanzo: BBC Swahili

Wanne wafariki kutokana na bomu Nigeria




Bomu lawauwaa watu wane Nigeria


Ripoti kutoka Nigeria zinasema kuwa mlipuaji wa kujitolea muhanga amewaua watu wanne na kuwajeruhi wengine kadhaa katika shambulizi la kituo cha basi huko Potiskum.
Mji huo umekuwa ukishambuliwa na wapiganaji wa boko haram kwa mara kadhaa sasa.
Jumapili iliopita walipuaji wawili wa kujitolea muhanga walijilipua na kuwaua watu wanne katika soko moja lililojaa watu.
Wachanganuzi wanakadiria kwamba hadi watu elfu 13 wamefariki tangu kundi la boko haram lianzishe harakati zake mnamo mwaka 2009.

Chanzo: BBC Swahili

Mwanablogu taabani baada ya kichapo

 
Mwanablogu Raif Badawi ana majeraha ambayo hayawezi kumruhusu kupewa adhabu nyingine
 
Mwanablogu huyo ambaye pia ni mwanaharakati aliyeanzisha mtandao wa 'Forum Liberal Saudi Network' ambao sasa umefungwa na serikali, alitarajiwa kuchapwa viboko 50 hadharani baada ya sala ya Ijumaa hii leo.
Mwezi Mei mwaka jana, alihukumiwa miaka 10 jela na kuandikiwa adhabu ya mijeledi 1,000 kwa kuitusi dini ya kiisilamu pamoja na kutoitii sheria.
Bwana Badawi alipokea awamu ya kwanza ya viboko Ijumaa iliyopita huku kesi yake ikisababisha tuhuma kutoka kwa jamii ya kimataifa dhidi ya Serikali ya Saudia


Watetezi wa Raif Badawi
Hata hivyo serikali haikutoa tamko lolote kwa kukosolewa.
Kadhalika serikali hio ingali kutoa tamko kuhusu afya ya mwanablogu huyo na pia kuhusu kuahirishwa kwa adhabu yake.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu ikiwemo Amnesty International yamesema katika taarifa yao kwamba Badawi alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na kugundua kwamba uchungu na majereha aliyoyapata kutoka kwa mijeledi ya kwanza bado hazijapona.
Daktari wake alishauri adhabu yake kuahirishwa hadi atakapopata nafuu


Chanzo: BBC Swahili.