Mwanablogu taabani baada ya kichapo
![]() |
Mwanablogu Raif Badawi ana majeraha ambayo hayawezi kumruhusu kupewa adhabu nyingine |
Mwezi Mei mwaka jana, alihukumiwa miaka 10 jela na kuandikiwa adhabu ya mijeledi 1,000 kwa kuitusi dini ya kiisilamu pamoja na kutoitii sheria.
![]() |
Watetezi wa Raif Badawi |
Kadhalika serikali hio ingali kutoa tamko kuhusu afya ya mwanablogu huyo na pia kuhusu kuahirishwa kwa adhabu yake.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu ikiwemo Amnesty International yamesema katika taarifa yao kwamba Badawi alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na kugundua kwamba uchungu na majereha aliyoyapata kutoka kwa mijeledi ya kwanza bado hazijapona.
Daktari wake alishauri adhabu yake kuahirishwa hadi atakapopata nafuu
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment